1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kaskazini yataka kuimarisha uhusiano wake na Urusi

21 Januari 2024

Korea Kaskazini imesema imeridhia kuimarisha uhusiano wa kimkakati na Urusi, kuanzisha kile kilichoitwa ''mfumo mpya utakaozipa nguvu nchi nyingi ulimwenguni.''

https://p.dw.com/p/4bVcu
Korea Kaskazini | Sergei Lavrov mjini Pjöngjang
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov akiwa na mwenzake wa Korea Kaskazini  Choe Son Hui mjini PyongyangPicha: Russian Foreign Ministry/REUTERS

Hilo linafanyika katika wakati ambapo nchi hizo mbili zikishirikiana kujenga mshikamano wa kukabiliana na maadui zao kufuatia kuongezeka kwa mvutano na Marekani. 

Akielezea mkutano wake wa wiki iliyopita na rais wa Urusi Vladimir Putin pamoja na waziri wake wa mambo ya nje Sergei Lavrov mjini Moscow, Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini  Choe Son Hui amesema Putin alimhakikishia kuwa yuko tayari kufanya ziara Pyongyang. 

Waziri wa Mambo ya nje wa Korea Kaskazini azuru Moscow

Korea Kaskazini imekuwa ikijaribu kuimarisha mahusiano yake na Urusi, baada ya kiongozi wake Kim Jong Un kuitembelea Urusi mwezi Septemba mwaka jana na kukutana na Putin. 

Kim anajaribu kujiondoa katika mtego wa kutengwa kidiplomasia na kuimarisha nguvu zake wakati akiendelea kupingana na Washinton,Seol na Tokyo kufuatia madai ya silaha za nyuklia.