SiasaKorea Kaskazini
Korea Kaskazini yarusha makombora mawili bahari ya mashariki
31 Agosti 2023Matangazo
Jeshi la Korea Kaskazini limesema katika taarifa kuwa, makombora hayo yalirushwa jana jioni katika kile kilichoelezwa kuwa ni "mazoezi ya kimkakati ya shambulio la nyuklia."
Shirika la habari la Korea Kusini la Yonhap, likinukuu jeshi la nchi hiyo kuwa, makombora hayo yalirushwa kuelekea bahari ya mashariki ambayo pia inafahamika kama bahari ya Japan.
Urushaji huo wa makombora - ulioripotiwa kwa mara ya kwanza na jeshi la Korea Kusini - umetokea katikati ya luteka za kijeshi za kila mwaka zinazofanywa na Marekani na Korea Kusini, na aghalabu kuikasirisha Pyongyang.
Jeshi la Korea Kaskazini limesema katika taarifa kuwa, urushaji wa makombora hayo unalenga kutuma ujumbe kwa maadui.
Pyongyang imefanya majaribio kadhaa ya makombora mwaka huu.