1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa upinzani Zimbabwe Sikhala aachiwa huru

31 Januari 2024

Mwanasiasa wa upinzani nchini Zimbabwe Job Sikhala, ambaye amekuwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja nanusu, ameachiliwa huru baada ya mahakama ya Harare kumpa kifungo cha nje.

https://p.dw.com/p/4brQi
Mabango ya kampeni za uchaguzi Zimbabwe
Mabango ya kampeni za uchaguzi ZimbabwePicha: Zinyange Auntony/AFP via Getty Images

Mkosoaji huyo mkubwa wa serikali mwenye umri wa miaka 51 alikuwa mmoja wa watu maarufu waliokamatwa katika miaka ya karibuni katika kile mashirika ya haki yameeleza kuwa ni ukandamizaji dhidi ya sauti za upinzani katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Sikhala amewaambia waandishi habari baada ya kuondoka katika gereza lenye ulinzi mkali viungani mwa mji mkuu Harare jana jioni kuwa watu waliomuweka jela kwa muda mrefu wanapaswa kuelewa kuwa dhamira yake ya kulipa gharama yoyote kwa upendo wa nchi yake haina aibu.

Mbunge huyo wa zamani, Sikhala alihukumiwa kwa kuchochea ghasia za umma wiki iliyopita baada ya kumalizika kwa kesi yake iliyodumu kwa mwaka mmoja na ambayo wafuasi wake walisema ilichochewa kisiasa.