1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis auomba Umoja wa Ulaya kuwa na mshikamano

22 Aprili 2020

Kiongozi Mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameutolea mwito Umoja wa Ulaya kubaki na mshikamano katika kukabiliana na athari za janga la virusi vya Corona.

https://p.dw.com/p/3bFgd
Vatikan | Papst Franziskus während Ostermesse im Petersdom
Picha: Getty Images/AFP/A. Solaro

Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki, ametowa mwito huo siku moja kabla ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya utakaojadili mpango mkubwa wa kiuchumi.

Janga la virusi vya Corona limesababisha mivutano mingine katika umoja huo wenye nchi wanachama 27, na kwa mara nyingine kuonekana migawanyiko kati ya nchi tajiri za Ulaya Kaskazini na zile masikini kabisa za upande wa Kusini.

Kadhalika Papa Francis ameuomba Umoja wa Ulaya kusali ili ufanikiwe kuuendeleza mshikamano wao wa miaka mingi. Ni mara ya pili katika kipindi cha siku 10 kwa Papa Francis ambaye ni muungaji mkono mkubwa wa Umoja wa Ulaya kuzungumzia wasiwasi wake kuhusu Jumuiya hiyo.