1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Kiongozi wa Hamas afanya ziara Tehran

29 Machi 2024

Mnadhimu Mkuu wa jeshi la Iran Jenerali Mohammed Bagheri ametembelewa na kiongozi wa wanamgambo wa Hamas Ismail Haniyeh mjini Tehran wakati kundi hilo likiendelea na mapambano yake dhidi ya Israel katika ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4eG8z
Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei na Ali Khamenei kiongozi wa kundi la Hamas
Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei na Ali Khamenei kiongozi wa kundi la Hamas Picha: Irna

Takriban miezi sita baada ya mzozo huo kuanza mnamo Oktoba 7 kati ya Israel na Hamas, Jenerali Bagheri alisifu vita vya kundi hilo dhidi ya Israel. Aliyaelezea mauaji ya watu wa Israel ya mwezi Oktoba yaliyoanzisha mgogoro unaendelea kwa sasa Mashariki ya Kati, kama jambo jambo zuri lililoyaweka matakwa ya watu wa palestina mbele na kujulikana dunia nzima.

Hii ni ziara ya pili ya Haniye nchini Iran tangu mapigano hayo yalipoanza. Iran inasemekana kuwaunga mkono wanamgambo wa Hama walioorodheshwa kama kundi la kigaidi na Umoja wa Ulaya, Marekani na Israel.