Kesi ya udhalilishaji watoto kingono kurindima mjini Koeln
10 Agosti 2020Katika uchunguzi huo wa uhalifu wa udhalilishaji watoto wadogo kingono kupitia mtandao wa kihalifu, washukiwa 10,000 wamechunguzwa. Leo inaanza kesi dhidi ya uhalifu huo mjini Koeln .
Picha za ngono na vidio , ambazo polisi ilizipata kwa mtu huyo Joerg L mwenye umri wa miaka 43, pamoja na mazungumzo yake na kundi la siri la watu waliojipa majina ya bandia kama Lila06789 Homer Simpson, au Bullseye, zinaelekeza katika uchunguzi mpana wa matumizi ya nguvu dhidi ya watoto katika historia ya jamhuri ya Ujerumani.
Soma pia Udhalilishaji wa watoto Ujerumani watisha
Uchunguzi huo ulifanyika katika nyumba ambayo inaonekana ni makaazi salama ya familia. Majirani wakiieleza kuwa familia nzuri na ya kawaida kwa nje, katika mji wa Bergisch Gladbach, kama anavyokumbuka Lisa Wagner polisi aliyekuwapo siku hiyo ya uchunguzi , asubuhi ya tarehe 21 , Oktoba 2019.
Kiasi ya watoto 50 walipatikana katika nyumba hiyo, ikiwa ni pamoja na mtoto wa miezi mitatu. Orodha ya wahalifu hao waliotambulika imefikia watu 87, anasema Markus Hartmann katika ofisi ya waendesha mashitaka mjini Koeln, ambaye anaongoza kitengo cha uhalifu wa mitandaoni.
Udhalilishaji kingono
Kwa kila mmoja katika watu hao 87 kuna ushahidi mwingine unaopatikana, ambao ni watu wengine wanaofanya uhalifu huo. Mwendesha mashitaka Hartmann amesisitiza kwamba:
"Hatukuwa tunajishughulisha na mtu mmoja tu, badala yake wahalifu walikuwa na mawasiliano mazuri, ambayo yaliwezesha wao kufanya uhalifu huo, na kufanikiwa kuuficha."
Soma pia Udhalilishaji watoto bado tatizo duniani
Uwezekano huu wa mawasiliano ndio ulikuwa msingi mkubwa wa udhalilishaji huu kingono. Mwishoni mwa mwezi Juni waziri wa sheria wa jimbo la North Rhine Westfalia Peter Biesenbach, kwamba wachunguzi wamepata majina na waliko zaidi ya wahalifu 30,000. Biesenbach anazungumzia kuhusu kiwango cha uhalifu huo, unaokera. Wachunguzi wanazungumzia kuhusu makundi ya mawasiliano , ambapo kuna watu zaidi ya 1,800 wanaofanya mawasiliano, kama anavyoeleza Markus Hartmann.
"Ukiangalia kwa kina kuhusu mawasiliano hayo, utaona kwamba washiriki wa mazungumzo hayo wanatambua kuwa uhalifu dhidi ya watoto ni suala lisilokubalika katika jamii."
Soma pia Mapadri wahusishwa na udhalilishaji kingono Marekani
Utambuzi kwamba, kuna adhabu kali kwa watu wanaofanya uhalifu huo, ulionekana katika mawasiliano yao wakionekana kama watu wa kawaida katika jamii. Lakini hata hivyo watu hao kila mara waliendelea na uhalifu huo.