JamiiNigeria
Watu wasiopungua 59 wafariki kwa moto nchini Nigeria
9 Septemba 2024Matangazo
Msemaji wa shirika la dharura wa eneo hilo Ibrahim Husseini, amesema idadi ya waliokufa katika ajali hiyo iliyotokea Jumapili asubuhi imeongezeka na kufikia 59, kutoka 52 za mapema Jumatatu na tayari wamezikwa.
Katika ajali hiyo, ng'ombe 50 pia waliungua kwa moto baada ya lori la mafuta.
Milipuko ya malori yanayobeba mafuta imekuwa ikitokea mara kwa mara Nigeria ambapo barabara za taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika hazifanyiwi ukarabati ipasavyo.
Wakati wa ajali za aina hiyo, wakaazi wa maeneo kunakotokea hukimbilia kukinga mafuta kutoka kwenye malori hayo.