1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 9 wamekufa Nigeria kutokana na ajali ya lori la mafuta

Daniel Gakuba
29 Juni 2018

Watu 9 wamekufa baada ya lori lililokuwa limebeba mafuta kupinduka na kuwaka moto mjini Lagos

https://p.dw.com/p/30X1k
Nigeria Explosion Pipeline
Picha: picture-alliance/ dpa

Maafisa wa Nigeria wamesema watu 9 wamekufa kutokana na ajali ya lori lililokuwa limebeba tanki la mafuta, ambalo lilipinduka na kuwaka moto kwenye daraja moja mjini Lagos.

Kitengo cha kushughulikia maafa mjini Lagos kimesema katika tangazo lake kwake miongoni wa waliokufa alikuwemo mtoto mchanga.

Ajali hiyo hali kadhalika iliwajeruhi watu wengine wanne, na magari 54 yaliungua moto. Bado hakuna maelezo zaidi kuhusu kilichosababisha ajali hiyo jana jioni jioni.

Shughuli zimeendelea katika eneo la ajali, kusafisha barabara na kuondoa magari yaliyoharibika.

Lagos ni mojawapo wa miji mikubwa kabisa barani Afrika, ukiwa na wakazi zaidi ya milioni 21. Nigeria inaongoza kwa uzalishaji wa mafuta katika bara la Afrika.