1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMisri

Watu 38 wajeruhiwa katika kisa cha moto, Misri

2 Oktoba 2023

Watu 38 wamejeruhiwa baada ya moto mkubwa kuripotiwa katika makao makuu ya polisi mjini Ismailia nchini Misri hii leo Jumatatu.

https://p.dw.com/p/4X2hc
Wanajeshi wakiimarisha usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 150 tangu kuzinduliwa kwa mfereji wa Suez katika mji wa Ismailia kulikotokea moto uliounguza jengo linalokaliwa na wanajeshi wengi.
Wanajeshi wakiimarisha usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 150 tangu kuzinduliwa kwa mfereji wa Suez katika mji wa Ismailia kulikotokea moto uliounguza jengo linalokaliwa na wanajeshi wengi.Picha: KHALED DESOUKI/AFP/Getty Images

Vidio zilizosambazwa katika vyombo vya habari zilionyesha moshi mkubwa mweusi ukitoka ndani ya makao makuu hayo. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

Wanajeshi 26 waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali iliokuwa karibu, 24 walipata matatizo ya kupumua huku wawili wakitibiwa majeraha ya moto. Wengine 12 walitibiwa katika eneo la tukio.

Kulingana na vyombo vya habari nchini humo, wizara ya afya imepeleka magari ya kubebea wagonjwa 50 katika eneo hilo zilizounganishwa na huduma za dharura za kijeshi zikiwemo ndege mbili za kijeshi.