1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiganaji watano wa Hamas wauwawa Kaskazini mwa Gaza

22 Novemba 2024

Jeshi la Israel limesema limewaua wapiganaji watano wa kundi la Hamas ikiwa ni pamoja na makamanda wake, katika mashambulizi ya usiku kucha kwenye mji wa Beit Lahiya ulio Kaskazini mwa Gaza.

https://p.dw.com/p/4nJEa
Beit Lahiya, Ukanda wa Gaza
Sehemu ya eneo la Beit Lahiya iliyoathiriwa na mashambulizi ya anga ya IsraelPicha: AFP

Taarifa iliyotolewa na jeshi na shirika la Ujasusi la Israel Shin Bet siku ya Ijumaa, imesema wamewaangamiza wanamgambo hao akiwemo kamanda wa tawi la kijeshi la Hamas la Al-Qassam Brigades pamoja na kamanda mwingine wa ziada wa tawi hilo walioshiriki katika mauaji ya Oktoba 7 nchini Israel yaliosababisha kuzuka kwa vita vya Gaza mwaka jana. 

Soma zaidi: Wapalestina 15 wauawa na jeshi la Israel huko Gaza

Taarifa hiyo imeongeza kuwa makamanda hao waliouwawa waliongoza  mauaji  na utekaji nyara katika eneo la Mefalsim, la jamii ya kibbutz, kusini mwa Israel karibu na mpaka wa Gaza.  Madaktari wa Palestina wamesema makumi ya watu wameuwawa wakati wa mashambulizi hayo.

Jeshi la Israel imeendelea kufanya operesheni zake Gaza ikiwa ni siku moja baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu - ICC kutoa waranti wa kukamatwa kwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.