1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, Messi atabeba tena Ballon d'Or?

30 Oktoba 2023

Lionel Messi apewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo yake ya nane ya mchezaji kandanda bora duniani FIFA Ballon d'Or.

https://p.dw.com/p/4YCie
Fußball Ballon d'Or
Tuzo ya Ballon d'OrPicha: Benoit Tessier/REUTERS

Lionel Messi anapewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo yake ya nane ya FIFA Ballon d'Or wakati sherehe za mwaka huu za mwanasoka bora zitakapofanyika mjini Paris leo Jumatatu.

Tuzo hiyo ya kifahari imetawaliwa zaidi ya miaka 15 iliyopita na Messi na mpinzani wake wa zamani Cristiano Ronaldo, ambao wameshinda mara 12 kati yao huku Luka Modric na Karim Benzema wakishinda mara moja kila mmoja.

Soma pia: Messi aeleza kilichochangia kushinda Ballon d'Or

Katika orodha ya kushindania taji hilo kuna wachezaji saba wa timu ya Manchester City iliyoshinda Ligi Kuu ya England, Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa Ulaya chini ya kocha Pep Guardiola. Wa kwanza kati ya wachezaji wa Manchester City katika orodha hiyo ni Erling Haaland, ambaye alifunga mabao 52 katika mechi 53 na tayari ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Shirikisho la Kandanda Ulaya UEFA kwa msimu uliopita.

Soma pia: FIFA yatoa orodha ya walioteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2023

Nani mkali kwa upande wa wanawake?

BG Beste Fußballerinnen der Welt
Aitana Bonmati katika mechi kati ya Barcelona and Olympique Lyon ndani ya uga wa Allianz Stadium Mei 21, 2022 huko Turin Italia.Picha: Marco Canoniero/Sportphoto24/picture alliance

Kwa upande wa wanawake orodha ya walioteuliwa inawajumuisha wachezaji wanne wa timu ya Uhispania ambayo ilinyakua Kombe la Dunia la Wanawake huko Sydney mnamo Agosti.

Alba Redondo, Salma Paralluelo na beki wa pembeni Olga Carmona, wote wameorodheshwa, lakini Aitana Bonmati anaonekana kuwazidi wenzake.

Huku haya yakijiri Shirikisho la kandanda duniani, FIFA, hii leo limetangaza kuwa limempiga marufuku ya miaka mitatu rais wa zamani wa shirikisho la kandanda wa Uhispania Luis Rubiales kufuatia sakata la kumbusu mdomoni pasipo na idhini mchezaji wa timu ya taifa ya Uhispania ya wanawake Jenni Hermoso.

Luis Rubiales
Luis RubialesPicha: Denis Balibouse/REUTERS

Soma pia:Hermoso akanusha kutoa ridhaa ya kupigwa busu na Rubiales 

Katika taarifa yake kamati ya nidhamu ya FIFA imesema imemfungia Rubiales, kwa shughuli zote zinazohusiana na kandanda katika ngazi ya kitaifa na kimataifa kwa miaka mitatu. Na kwamba tayari Rubiales amearifiwa kuhusu uamuzi huo na ana siku 10 za kukata rufaa.

Tazama pia picha na melezo za: