1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaendeleza mshambulizi eneo la Ukingo wa Magharibi

30 Agosti 2024

Jeshi la Israel limefanya mashambulizi ya angani katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu wakati operesheni yake kubwa ya kijeshi ikiingia siku ya tatu, huku ripoti zikisema Wapalestina wasiopungua 16 wameuawa.

https://p.dw.com/p/4k6Wn
Ukingo wa Magharibi | Mashambulizi ya Israel
Gari lililoteketea kwa moto baada ya mashambulizi ya Israel katika eneo la Ukingo wa Magharibi.Picha: Raneen Sawafta/REUTERS

Israel imedai mashambulizi hayo operesheni yake kwenye miji na kambi za wakimbizi kote kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi kuwa ni ya kupambana na ugaidi.

Mwandishi wa shirika la habari la AFP ameripoti miripuko mikubwa na moshi katika kambi ya wakimbizi mjini Jenin. 

Vikosi vya Israel viliondoka kwenye miji mingine ya Ukingo wa Magharibi jana jioni, lakini mapigano yameendelea karibu na Jenin, ambako kwa muda mrefu kumekuwa kitovu cha harakati za wapiganaji.

Soma pia:Vikosi vya Israel vyawauwa Wapalestina wanane Ukingo wa Magharibi

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa operesheni hiyo iliyoanzishwa Jumatano, inachochea hali ambayo tayari ni tete na kuitaka Israel kuikomesha mara moja.