1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yatishia kurejea katika matumizi ya nyuklia

Sudi Mnette Mohammed Khelef
9 Mei 2019

Umoja wa Ulaya na mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Ufaransa na Uingereza wamesema bado wanayazingatia makubaliano ya nyuklia ya Iran lakini hawakubaliani na muda wa mwisho uliotolewa na Iran.

https://p.dw.com/p/3IDjg
Iran l Teilausstieg aus dem Atomabkommen - Atomkraftwerk in Buschehr
Picha: picture alliance/AP Photo

Taarifa ya pamoja ya wadau hao inasema haikubaliani na muda uliowekwa na Iran na kwamba watalifutalia kwa kina taifa hilo katika kusimamia utekezaji wa makubaliano ya nyuklia kwa mujibu wa miongozo ya kanuni za usimamizi za kimataifa. Wamesema wamesikitishwa na kitendo cha Marekani kuliwekea tena vikwazo taifa hilo baada ya Rais Donald Trump kujiondoa katika makubaliono ya nyuklia na kuongeza kwamba wataendelea kuwa thabiti kuyalinda na kuyatekeleza makubalino ya mpango ya nyuklia wa Iran.

Kwa kauli moja wamesisitia kuitaka Iran kuendelea kuyatekeleza majukumu yake kwa ukamilifu  kama ilivyo sasa, chini ya makubaliano ya JCPOA, yaani mpango wa utekelezaji wa pamoja ambao unafahamika pia kama mpango ya nyuklia. Na kujiepusha kabisa na hatua yoyote itakayoweza kuyavuruga. Aidha wameyataka mataifa ambayo hayamo katika mpango huo, kufanya vitendo vyovyote ambavyo vitaathiri uwezo wa mataifa yanayoshiriki kufanikisha majukumu yao.

Taarifa ya kujiondoa katika makubaliano ya Iran

Irak Staatsbesuch Hassan Rohani
Rais wa Iran Hassan RohanPicha: picture-alliance/AA/Iranian Presidency

Awali hivi leo, Baraza la Usalama wa Taifa la Iran lilisema nchi hiyo itaanza kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 ambayo yanaizuia Iran isitengeneze silaha za nyuklia, kama mataifa hayo makubwa washirika katika makubaliano hayo hayatatoa unafuu kwa kuliondelea vikwazo taifa hilo kama walivyokubaliana. Mataifa mengine mbali na ya Ulaya ambayo yanajumuika katika mpango huo ni China na Urusi.

Kiongozi wa chama cha mrengo wa kati kulia, EPP, katika bunge la Ulaya, Manfred Weber, amesema kauli hiyo ya Iran haitoi matumaini ya kupunguza mvutano. Na kuongeza kusema Umoja wa Ulaya lazima uwe kiini cha diplomasia, na lazima utafute njia nzuri ya kutatua matatizo. Kauli ya Iran haiwezi kusaidia. "Nafikiri a Umoja wa Ulaya lazima uanze tena mazungumzo na marafiki zetu wa Iran, kwa sababu hatutaki kuona aina yoyote ya mivurugano ya kikanda."

Iran ilitangaza kuchukua hatua zaidi, kama mataifa hayo ya Ulaya yatashindwa kutimiza wajibu wake wa kupunguza athari za vikwazo ilivyowekea taifa hilo katika kipindi cha siku 60 zijazo. Maeneo ambayo yameathirika zaidi ni sekta za uzalishaji mafuta na kibenki.

Hata hivyo mtaalamu kutoka mtandao wa European Leadership Network unaojihusisha na masuala ya sera barani Ulaya, Axel Hellman, anasema Iran bado haijachukua hatua yoyote hadi sasa ambayo inaweza kusababisha kitisho katika uendelezaji wake mkataba wa nyuklia.

Vyanzo:dpa/rtre