1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yaanza kuhesabu kura, wahafidhina wakitarajiwa kushinda

2 Machi 2024

Iran imeanza kuhesabu kura , baada ya uchaguzi wa bunge na baraza la uteuzi wa kiongozi mkuu wa taifa hilo, ambao vyombo vya habari vya ndani vinakaridiria uitikiaji mdogo na wahafidhina wakitazamiwa kuibuka na ushindi.

https://p.dw.com/p/4d6du
Teheran, Iran  | Ali Hosseini Khamenei
Kiongozi wa Juu wa Iran Ali Hosseini KhameneiPicha: Iranian Leader Press Office/Handout/AA/picture alliance

Uchaguzi huo wa jana Ijumaa ndiyo ulikuwa wa kwanza tangu maandamano makubwa yaliosababishwa na kifo cha mwanamke wa Kikurdi Mahsa Amini, mwenye umri wa miaka 22 mnamo mwezi Septemba, akiwa katika kizuwizi cha polisi wa maadili, kwa kosa la kukiuka kanuni ya mavazi.

Iran imeathirika vibaya kutokana na vikwazo vya kimataifa vilivyosababisha mzozo wa kiuchumi tangu uchaguzi uliyopita mwaka 2020. Rekodi ya wagombea 15,200 walikuwa wanawania nafasi katika bunge lenye jumla ya viti 290.

Soma pia:Ripoti zisizo rasmi zaonyesha karibu asilimia 40 walipiga kura Iran

Wagombea wengine 144 waliwania kuchaguliwa katika Baraza la Wataalamu lenye viti 88, ambalo linaundwa na wanazuoni wa kiume wa kidini tu.

Hata hivyo mashirika ya habari ya ndani yamesema uitikiaji ulikuwa zaidi ya asilimia 40 ya watu milioni 61 wenye vigezo vya kupiga kura.