Muitikio wa zoezi la upigaji kura Iran ni takriban 40%
2 Machi 2024Baada ya vigogo wengi wa siasa za wastani na wahafidhina kutoshiriki mchakato huo, ambao wanamageuzi waliutaja kuwa usio huru na wa haki, kinyang'anyiro kilibaki hasa miongoni mwa wanasiasa wenye msimamo mkali na wahafidhina wasio maarufu wanaotangaza utiifu kwa nadharia za mapinduzi ya Kiislamu.
Wizara ya Mambo ya ndani inatarajiwa kutangaza takwimu rasmi za uitikiaji baadae leo. Uchaguzi huo ulifanyika katika wakati hali ya kukata tamaa inazidi nchini Iran kuhusiana na madhila ya kiuchumi na ukandamizaji wa uhuru wa kisiasa na kijamii.
Soma pia:Iran yaandaa uchaguzi wa kwanza wa bunge tangu maandamano ya kuipinga serikali
Kura bunge iliunganishwa pia na kura ya Baraza la Wataalamu lenye viti 88, ambalo lina jukumu la kuchagua mrithi wa Kiongozi wa Juu ya taifa hilo Ali Khamenei, mwenye umri wa miaka 84 sasa.