SiasaIran
Iran kufanya mazungumzo ya Nyuklia na mataifa ya Ulaya
24 Novemba 2024Matangazo
Iran imetangaza kuwa itafanya mazungumzo ya nyuklia na nchi tatu za Ulaya — Ufaransa, Ujerumani, na Uingereza — wiki ijayo mjini Geneva.
Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika Novemba 29 na yatahusu mzozo wa mpango wa nyuklia wa Iran, kufuatia azimio lililopitishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la udhibiti wa nyuklia dhidi ya Iran. Iran ilijibu azimio hilo kwa hatua kama vile kuwasha vinu vipya na vya kisasa vya urutubishaji wa urani.
Serikali ya Rais Masoud Pezeshkian inatafuta suluhu ya mkwamo wa nyuklia kabla ya kuapishwa kwa Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump, Januari.