Watu 43,000 wamepoteza makazi Libya kutokana na mafuriko
22 Septemba 2023Matangazo
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia uhamiaji (IOM) limesema zaidi ya watu 43,000 wamepoteza makazi yao nchini Libya kutokana na mafurikomakubwa.
Maelfu ya watu pia walikufa kwenye maafa. Mji wa Derna ndio ulioathirika ulioathirika zaidi na mafuriko hayo.
Shirika la IOM limesema mahitaji yanayotakiwa kwa haraka ni pamoja na chakula, maji ya kunywa na dawa na msaada wa kisaikolojia kwa wahanga.
Mapema wiki hii, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), lilitahadharisha juu ya hatari ya kuenea magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu kutokana na raia wa kulazimika kunywa maji machafu na pia kutokana na uhaba wa vyoo.