1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko yasababisha watu 43,000 kuyahama kaazi yao Libya

21 Septemba 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia uhamiaji (IOM) limesema zaidi ya watu 43,000 wameyakimbia makaazi yao Libya, kkufuatia mafuriko yaliyosababisha vifo vya maelfu ya watu mjini Derna.

https://p.dw.com/p/4Wf9G
 Internationaler Flüchtlingsorganisation IOM Logo
Picha: Steinach/IMAGO

Shirika la IOM limeongeza kuwa ukosefu wa maji unaoshuhudiwa kaskazini-mashariki mwa Libya, umewafanya raia wengi kuyahama makazi yao huko Derna na kwenda maeneo mengine. 

Mamlaka za Libya zimewataka wananchi kutotumia maji kutoka kwenye mtandao wa usambazaji, wakisema yamechafuliwa na mafuriko.

Mapema wiki hii, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), lilionya kuhusu hatari ya kuenea kwa magonjwa ya miripuko kama kipindupindu kutokana na raia wa Libya kutumia maji machafu na kukabiliwa na uhaba wa vyoo.