1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaIndia

India yaweka vizuizi baada ya wawili kufa kwa virusi- Nipah

14 Septemba 2023

India imezuia kikusanyiko ya umma na kuzifunga baadhi ya shule katika jimbo la Kerala kusini mwa taifa hilo baada ya watu wawili kufa kwa maambukizi ya virusi aina ya Nipah vinavyoambukizwa na popo ama nguruwe.

https://p.dw.com/p/4WKgk
Watu waliovamia mavazi ya kujikinga wakibeba mwili wa mtu aliefariki kwa virusi vya Nipah
Watu waliovamia mavazi ya kujikinga wakibeba mwili wa mtu aliefariki kwa virusi vya NipahPicha: Shijith. K/AP Photo/picture alliance

India imezuia kikusanyiko ya umma na kuzifunga baadhi ya shule katika jimbo la Kerala kusini mwa taifa hilo baada ya watu wawili kufa kwa maambukizi ya virusi aina ya Nipah vinavyoambukizwa na popo ama nguruwe na kusababisha homa kali.

Virusi hivyo havina chanjo na uwezo wake wa kusababisha kifo ni kati ya asilimia 40 hadi 75, hii ikiwa ni kulingana na Shirika la afya ulimwenguni, WHO.

Soma zaidi:India yaweka vizuizi baada ya kirusi cha Nipah kuuwa watu 2

Dalili za maambukizi ambazo hujitokeza baada ya siku 4 hadi 14 ni pamoja na homa, kutapika na maambukizi kwenye mapafu, ingawa maambukizi makali yanaweza kusababisha kifafa, ubongo kuvimba na pengine kuwekewa mashine ya kusaidia kupumua.

Watu wengine watatu wamekutwa na maambukizi na zaidi ya 700 ambao ni pamoja na wafanyakazi wa afya 153 waliokutana na waathirika wanafuatiliwa, maafisa wa afya wamesema.