Ibada ya Hajj yakamilika na kukaribisha Eid Ul Adha
16 Juni 2024Matangazo
Ibada hiyo ndio inakamilisha mwiso wa Ibada ya Hijja na kuanza kwa siku kuu ya Eid ul Adha inayosherehekewa na waislamu wote kote duniani.
Ibada hiyo imefanyika siku moja baada ya mahujaji zaidi ya milioni 1.8 kukusanyika na kufanya ibada katika mlima Arafa nje ya mji huo mtukufu wa makka.
Mahujjaji wakusanyika Arafat katika kilele cha Hijja
Baadae mahujaji waliondoka katika mlima huo jana Jumamosi jioni kulala katika eneo lililokaribu linalojulikana kama Muzdalifa ambapo walikusanya vijiwe vidogo na kuvitumia kama ishara ya kumpiga shetani katika nguzo zilizopo katika eneo jengine takatifu la Mina.
Waislamu walio na uwezo wanatarajiwa kufanya ibada hiyo mara moja kwa mwaka.