1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hochstein ziarani Israel kusaka suluhu ya Israel -Hezbollah

17 Juni 2024

Mjumbe wa Marekani Amos Hochstein yupo nchini Israel kujaribu kuzuwiya kutanuka kwa mzozo kati ya Israel na wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran, Hezbollah wanaoshambulia karibu na mpaka wa Kaskazini mwa Israel.

https://p.dw.com/p/4hA7u
Mjumbe wa Marekani Amos Hochstein
Mjumbe wa Marekani Amos HochsteinPicha: Houssam Shbaro/AA/picture alliance

Mwanadiplomasia hiyo aliwasili leo Israel kwa majadiliano ya kupata suluhu ya kidiplomasia kati ya pande hizo mbili. Taarifa zaidi zinasema Hochstein anapanga pia kufika Lebanon kujadili suala hilo na viongozi wa taifa hilo. 

Hii leo atakutana na waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu pamoja na Yoav Galant waziri wa ulinzi wa taifa hilo. Tangu kuanza kwa vita vya Gaza miezi minane iliyopita, kumekuwa na  mshambulizi ya kijeshi kati ya jeshi la Israel na wanamgambo wa Hezbollah huku kukiripotiwa vifo kwa pande zote mbili. 

Soma pia:Hezbollah yaendeleza mashambulizi ya kisasi dhidi ya Israel

Takriban watu 150,000 wamehamishwa au kuondoka wenyewe katika eneo hilo la mapigano.