Guterres akitembelea kivuko cha Rafah
20 Oktoba 2023Malori yaliyosheheni misaada ya kibinaadamu yameegeshwa karibu na kivuko hicho upande wa Misri.
Wakati vita vikiingia siku ya 14 siku ya Ijumaa (Oktoba 20), Hamas imesema Wapalestina wapatao 4,137 wameuawa huku wengine 13,000 wakijeruhiwa.
Israel inasema kundi la Hamas liliwaua watu 1,400 na kuwachukuwa mateka takribani 200 katika shambulio lao la Oktoba 7 ndani ya ardhi ya Israel.
Soma zaidi: Mashambulizi yaitikisa Gaza huku juhudi za kutuma misaada zikijikokota
Mataifa ya Kiarabu ya Ghuba na yale ya kusini mashariki mwa bara la Asia yamelaani leo hii mashambulizi dhidi raia na yametoa wito wa kusitishwa kwa vita kati ya Israel na Hamas na kuruhusu usafirishaji wa misaada ya kiutu kwa mamilioni ya watu kwenye Ukanda wa Gaza.
Viongozi mbalimbali duniani, akiwemo Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmud Abbas, watahudhuria mkutano wa kilele wa kusaka amani katika mzozo huo wa Mashariki ya Kati unaofanyika sikuj ya Jumamosi (Oktoba 21) mjini Cairo, Misri.