1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Greta Thunberg ahutubia mkutano wa COP25 mjini Madrid

Oumilkheir Hamidou
11 Desemba 2019

Mwanaharakati Greta Thunberg, amewakaariüpia wanasiasa na wanaviwanda kwa kutowajibika katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi katika mkutano wa Umoja wa Mataifa unaoendelea mjini Madrid,

https://p.dw.com/p/3UaaO
Madrid Klimakonferenz COP25 Greta Thunberg Luisa Neubauer
Picha: DW/J. Alonso

Mwanaharakati wa usafi wa mazingira, Greta Thunbergh anahudhuria mkutano wa viongozi wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mastaifa mjini Madrid akifuatana na mtaalamu wa sayansi ya mazingira Johan Rockstrom, waziri wa mazingira wa Uhispania Teresa Ribera na maafisa wengine wa ngazi ya juu.

Katika hotuba yake Greta Thunberg amelalamika na kusema "juhudi  za kupambana na mabadiliko ya tabianchi zinadorora." Mwanaharakati huyo wa usafi wa mazingira amewatuhumu wanasiasa na wafanyabiashara kujitafutia upenu wa kujisafishia hadhi zao badala ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Amesema kila mahala anakokwenda amegunduwa watu wanakosa mwaamko na miongoni mwa wanasiasa waliochaguliwa  hali ni mbaya zaidi. Greta Thunberg anasisitiza kwa kusema

Mwanaharakati mpigania usafi wa mazingira Greta Thunberg
Mwanaharakati mpigania usafi wa mazingira Greta ThunbergPicha: Imago Images/Agencia EFE

Greta Thunberg akosoa hadaa ya wanasiasa na wafanyabiashara

"Hatuna tena wakati wa kupuuza ishara zinazojitokeza. Kwa takriban mwaka mmoja sasa nimekuwa nikizungumzia kila wakati kuhusu kupungua bajeti ya kupambana na moshi wa carboni. Na kwakuwa watu hawazingatii hilo, na mie sina abudi isipokuwa kusema yale yale."

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 16 anasema hatari kubwa zaidi haitokani na ile hali ya kutofanya chochote, hatari kubwa zaidi inatokana na wanasiasa wanaoonyesha kana kwamba kuna kitakachotendeka katika wakati ambapo hakuna kinachotendeka.

Amenukuu ripoti za wanasayansi zinazozungumzia juu ya balaa linaloweza kuikumba dunia pindi hali ya ujoto duniani itaongezeka kwa nyuzi joto 1.5.

Kabla ya hapo katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres aliwahimiza viongozi wanaohudhuria mkutano huo wa mabadiliko ya tabianchi COP25 mjini Madrid waharakishe kufikia maendeleo mnamo siku hizi za mwisho mwisho za mkutano huo wa wiki mbili.