Umoja wa Ulaya wakubali kuiwekea Urusi vikwazo zaidi
25 Februari 2023Umoja wa Ulaya umekubaliana kuiwekea vikwazo vipya Urusi kufuatia vita vyake inavyoviendeleza Ukraine. Vikwazo hivyo vimewekwa hapo jana wakati vita hivyo vikiingia mwaka wake wa kwanza tangu vilipoanza tarehe 24 Februari 2022.
Vikwazo hivyo vimewalenga watu na kampuni binfasi wanaounga mkono vita hivyo, kueneza habari za propaganda kuvihusu au hata kupeleka ndege zisizokuwa na rubani zinazotumika na Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine.
Dunia yaungana na Ukraine kuilaani Urusi
Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, amesema bidhaa zitakazowekewa vikwazo Urusi ni pamoja na vifaa vya elektroniki, mashine ambazo huenda zikatumika katika utengenezaji wa ndege zisizokuwa na rubani za Urusi, makombora, helikopta na mifumo mengine ya silaha.
Hata hivyo vikwazo hivyo vinatarajiwa kuidhinishwa leo iwapo hakutakuwa na taifa hata moja la Umoja huo litakalopinga hilo.