China:Tutaimarisha ushirikiano na Urusi 2023
26 Desemba 2022Wang amesema China itazingatia mikakati ya kuaminiana na- ushirikiano na nurusi kwa manufaa kwa pande zote mbili.
Meli za kivita kutoka kwa nchi hizo mbili zilifanya mazoezi ya pamoja ya majeshi yao ya wanamaji katika Bahari ya mashariki ya China wiki iliyopita.
Wang, aliyazungumza hayo katika mkutano uliofanyika kwa njia ya video kwenye mji mkuu wa China, Beijing ambapo pia ameilaumu Marekani kutokana na kuzorota kwa uhusiano kati ya mataifa hayo mawili makubwa kiuchumi duniani.
Wang amesema China inapinga vikali sera mbaya ya Marekani dhidi yake pia ametaja kwamba shinikizo la nchi za magharibi dhidi ya nchi hiyo.
Soma pia:China, India zaigeuzia mgongo Urusi
China inataja shinikizo kubwa katika maswala ya biashara, teknolojia, haki za binadamu na kupinga hatua ya nchi hiyo kutangaza kulidhibiti eneo zaidi la magharibi mwa bahari ya Pasifiki ni hatua za uonevu za Marekani kutokana na China kukataa kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na hatua yake ya kukataa kuungana na nchi nyingine katika kuiwekea Urusi vikwazo.
Wang amesema sababu hizo zimechochea mivutano inayoendelea kujitokeza kati ya China na sehemu kubwa ya nchi za Ulaya.
Mazungumzo ya simu ya Wang na Blinken
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi alizungumza na mwenzake wa Marekani Antony Blinken kwa njia ya simu mwishoni mwa juma.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema Blinken amezungumzia juu ya kusimamia uhusiano baina ya mataifa hayo kwa kuwajibika na alielezea wasiwasi wake juuya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine unaoathiri vibaya usalama na utulivu wa uchumi wa dunia.
Soma pia:China yaitaka Marekani kuacha kukandamiza maendeleo yake
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Wang ameilaumu Marekani kwa kupendelea upande mmoja amesema hata hivyo amesema China itaendelea kuchukua jukumu muhimu la kuutatua mgogoro wa Ukraine kwa njia yake yenyewe.
: