1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiChina

China yaapa kushughulikia maadui katikati mwa maandamano

30 Novemba 2022

Chama tawala cha Kikomunisti nchini China kimeapa kushughulikia ipasavyo kile kilichokiita shughuli za kujipenyeza na uhujumu za maadui, kufuatia maandamano makubwa zaidi ya mitaani katika miongo kadhaa.

https://p.dw.com/p/4KHlw
China I Corona-Proteste in Guangzhou
Picha: REUTERS

Chama tawala cha Kikomunisti nchini China kimeapa kushughulikia ipasavyo kile kilichokiita shughuli za kujipenyeza na uhujumu za maadui, kufuatia maandamano makubwa zaidi ya mitaani katika miongo kadhaa, yaliofanywa na raia waliochoshwa na vizuizi vikali vya kupambana na UVIKO-19.

Tamko kutoka Kamisheni Kuu ya masuala ya kisiasa na kisheria, lililotolewa jana usiku, linakuja katikati mwa uoneshaji mkubwa wa nguvu na vikosi vya usalama kuzuwia kurejea kwa maandamano yaliozuka mwishoni mwa wiki mjini Beijing, Shanghai, Guangzhou na miji kadhaa mingine.

Wakati Kamisheni hiyo haikuyataja moja kwa moja maandamano, taarifa hiyo imechukuliwa kama ukumbusho juu ya azma ya chama hicho kudumisha utawala wake.