1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yataka kutatua utata mkataba wa nyuklia wa Iran

14 Februari 2023

Rais wa China Xi Jinping ametoa wito wa usuluhishaji wa makubaliano ya nyuklia ya Iran wakati akionyesha kuiunga mkono Jamhuri hiyo ya Kiislamu kulinda na kutetea haki yake pamoja na maslahi yake.

https://p.dw.com/p/4NTYQ
Besuch von Irans Präsident Raisi in China
Picha: Iranian Presidency/dpa/picture alliance

Xi alimwabia rais wa Iran Ibrahim Raisi aliyeanza ziara ya siku tatunchini humo, kwamba China itaendelea kushirikiana kikamilifu katika mazungumzo ya kuyafufua mazungumzo ya kurekebisha mkataba wa makubaliano ya nyuklia ya Iran.

Kabla ya kuanza ziara yake, Rais wa Iran amesema mataifa yote mawili yanaamini kwamba siasa za upande mmoja na kuwekewa vikwazo ni mambo yanayosababisha migogoro na kudorora kwa usalama duniani. 

Soma pia:Rais wa Iran ziarani China

Iran na China zina uhusiano imara wa kiuchumi, hasa katika nyanja za nishati, usafiri, kilimo, biashara na uwekezaji, na mwaka 2021 zilisaini mkataba wa miaka 25 wa ushirikiano wa kimkakati.