1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yahimiza kuundwa kwa dola la Palestina

21 Januari 2024

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa China Wang Yi ametoa wito wa kuundwa dola la Palestina na kutaka mapigano yasitishwe mjini Gaza, ambako siku 100 za vita kati ya Israel na Hamas zimesababisha mauaji ya maelfu ya watu.

https://p.dw.com/p/4bVoW
China | Wang Yi
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa China Wang YiPicha: Ahn Young-joon/AFP

Katika mkutano na mwenzake wa Misri Sameh Shoukry mjini Cairo, Wang Yi amesema ni muhimu kusisitizwa kuundwa kwa dola huru la Palestina kwa kuzingatia mipaka ya mwaka 1967 na Jerusalem kuwa mji wake mkuu. 

Taarifa ya pamoja kutoka kwa mawaziri hao wawili imehimiza kusitishwa mara moja vurugu, kuwauwa na kuwalenga raia na mali za raia wa Palestina. 

Kiongozi wa Hamas afanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uturuki

Wang aliuzungumzia mzozo huo wa Mashariki ya kati na rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi na pande zote mbili zilikubaliana kuwa usitishwaji wa mapigano unapaswa kufikiwa hara iwezekanavyo  ili kuzuwia mgogoro huo kusambaa katika maeneo mengine ya kikanda.