China na Marekani zatakiwa kupunguza mvutano wa kibiashara
23 Aprili 2020Matangazo
Wizara hiyo pia imeyataka mataifa yote mawili kuepuka kuwekeana vikwazo vipya vya biashara na uwekezaji. Msemaji wa wizara hiyo ya ya Biashara ya China Gao Feng, ameuambia mkutano wa habari kuwa mataifa hayo mawili yanapaswa kujongeleana, kuongeza ushirikiano na kusimamia tofauti zao.
Amesema hatua hizo ni muhimu katika kufufua uchumi wa dunia ulioathiriwa vibaya na mzozo wa janga la virusi vya corona.
China inapanga kununua zaidi tani milioni 30 za mazao ya kilimo kuisaidia kujilinda dhidi ya vurugu zilizotokea katika mfumo wa ugavi kutokana na janga la corona, na pia kutimiza ahadi ya kununua mazao zaidi kutoka Marekani.