China kupunguza gesi zinazochafua mazingira
4 Desemba 2007China katika mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa unaofanywa kisiwani Bali, Indonesia imesema,inatazamia kupunguza uzalishaji wa gesi zinazochafua mazingira,kwa kiwango kilichopendekezwa na nchi tajiri zilizoendelea kiviwanda.Imesema,itapunguza gesi hizo kutoka asilimia 25 hadi asilimia 40 ifikapo mwaka 2020. Mashirika yanayolinda mazingira,yamefurahia tangazo la China.
Kwa upande mwingine,mjini Brussels,Kamisheni ya Umoja wa Ulaya imesifu hatua iliyochukuliwa na Australia kutia saini mkataba wa Kyoto.Sasa Marekani ni nchi pekee tajiri kukataa kutia saini mkataba huo.
Kiasi ya wajumbe 10,000 kutoka nchi 190 wanahudhuria mkutano wa Bali,kujadili mkataba mpya wa hali ya hewa utakaochukua nafasi ya ule wa Kyoto unaomalizika mwaka 2012.