Chama cha upinzani Senegal kimelaani mauaji ya waandamanaji
5 Juni 2023Chama hicho kimedai kwamba serikali ilipeleka kile ilichokiita ''wanamgambo mamluki'' na kuwataka watu wachukue hatua ya kujitetea kwa namna yoyote na kukabiliana.
Kadhalika wafuasi wa Ousmane Sonko jana walilaani ukatili wa polisi baada ya kuzuka makabiiano wiki iliyopita kufuatia hatua ya kuhukumiwa kwenda jela miaka miwili kiongozi huyo wa upinzani, katika kesi ambayo anasema ilitengenezwa kumzuia kugombea kwenye uchaguzi wa rais wa mwaka ujao.
Soma pia: Upinzani Senegal waandamana kupinga uwezekano wa rais kuwania muhula wa tatu
Watu 16 waliuwawa kufuatia vurugu hizo na zaidi ya waandamanaji 350 walijeruhiwa. Jana serikali mjini Dakar, iliamua kuzima kwa muda data za intaneti za mawasiliano ya simu za mkononi, ikisema watu wanasambaza ujumbe wa chuki na uchochezi.