1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Chama cha Conservative cha Uingereza chafanya Mkutano Mkuu

1 Oktoba 2023

Chama tawala nchini Uingereza cha Conservative kinafanya mkutano wake mkuu kuanzia leo kikinuia kuupiga jeki umaarufu wake miongoni mwa umma kiasi mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu unaobashiriwa kuwa kitaupoteza.

https://p.dw.com/p/4X15c
Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak
Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak Picha: Kin Cheung/AP/dpa/picture alliance

Mkutano huo wa siku nne kwenye mji wa kaskazini magharibi wa Manchester, utakuwa wa kwanza kwa waziri mkuu Rishi Sunak aliyeingia madarakani Oktoba mwaka jana na huenda ni mwisho kabla ya uchaguzi ujao.

Sunak atajaribu kuutumia mkutano huo kuhuuisha haiba ya chama chake kilichopoteza umaarufu kwa wapiga kura kutokana na changamoto za kiuchumi na kupanda kwa gharama za kuendesha maisha.

Chama kikuu cha upinzani cha Labour ambacho kitafanya mkutano wake mkuu wiki ijayo, kinaongoza kura za maoni kwa tarakimu mbili zaidi ya Conservative, mwenendo unaokifungulia njia ya kurejea madarakani uchaguzi ujao