Chama cha CDU chakutana kuelekea uchaguzi wa kiongozi wao
15 Januari 2021Kura hiyo ni hatua muhimu kuelekea kumchagua mrithi wa Merkel. Kufikia sasa haijabainika ni nani aliye kifua mbele katika kinyang'anyiro cha kuwania uongozi wa chama hicho.
Kuna wagombea watatu, Armin Laschet ambaye ni waziri mkuu wa jimbo lenye idadi kubwa zaidi ya watu Ujerumani North Rhine-Westphalia, Wakili Friedrich Merz na mtaalam wa sera za kigeni Norbert Röttgen.
Laschet anaweka msisitizo zaidi katika haki za kijamii na usalama wa ndani.
"Je, chama chetu kinaiwakilisha jamii, jawabu ni hapana. Tukifanikiwa kuwavutia wahamiaji basi hapo tutakuwa na nafasi ya kusalia kuwa chama cha watu."
Kura hiyo inakuja katika mwaka muhimu sana kwa Ujerumani kwani uchaguzi wa kitaifa unatarajiwa kufanyika mwezi Septemba.
Merkel amepanga kustaafu kutoka kwenye siasa mwishoni mwa muhula wake huu ambao ni wa nne.