BRUSSELS: Ulaya ipunguze uchafuzi wa mazingira
30 Novemba 2006Matangazo
Halmashauri ya Umoja wa nchi za Ulaya inasema wanachama wake hawachukuwi hatua za kutosha kupunguza gesi zinazochafua mazingira.Halmashauri hiyo imewawekea wanachama wapya 10,vipimo vipya kwa azma ya kutekeleza malengo yaliokubaliwa katika Mkataba wa Kyoto,ili kupunguza uongezaji wa joto duniani.Umoja wa Ulaya kwa wastani, umewapunguzia wanachama wake,kwa asili mia 7 kile kipimo cha gesi ya kaboni dayoksaidi inayorouhusiwa kuanzia mwaka 2008 hadi 2012,ili mfumo huo uweze kufanya kazi kwa mafanikio. Ujerumani,iliyo mchafuzi mkubwa imesema,vipimo vikali hawiwezi kukubaliwa na kwamba hatua hiyo itaongeza bei ya nishati.