Bremen. SPD kuunda serikali na chama cha walinzi wa mazingira Greens.
21 Mei 2007Matangazo
Chama cha Social Democratic katika jimbo la Bremen nchini Ujerumani kimesema jana Jumapili kuwa wanatafuta kuunda serikali ya jimbo hilo pamoja na chama cha walinzi wa mazingira cha Green kufuatia ushindi wao katika uchaguzi wa hivi karibuni wa jimbo hilo.
Uamuzi huo unakuja baada ya chama cha Christian Democratic Union CDU kukataa kuendeleza muungano na chama cha Social Democratic , uliokuwapo tangu mwaka 1995.
Chama cha SPD kimepata asilimia 36.8 ya kura katika uchaguzi wa May 13 katika jimbo hilo na CDU kilipata asilimia 25.6.
Uongozi wa SPD umekubaliana jana Jumapili kutafuta muungano na chama cha Greens, ambao wamepata asilimia 16.4 ya kura, ameeleza Uwe Beckmeyer ambae ni rais wa chama hicho katika jimbo la Bremen.