1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Nchi za viwanda zipunguze zaidi uchafuzi wa mazingira

5 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMK

Serikali ya Ujerumani,katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya utakaofanywa juma lijalo mjini Brussels,itapendekeza kuwa ifikapo mwaka 2050, uchafuzi unaosababishwa na gesi ya kaboni dayoksaidi,upunguzwe na nchi zilizoendelea kiviwanda kwa asilimia 60 hadi 80.Kiwango hicho ni zaidi ya kile kilichoshauriwa na Halmashauri ya Umoja wa Ulaya kwamba hadi mwaka 2020,uchafuzi wa gesi hiyo upunguzwe kwa asilimia 20. Inasemekana,pendekezo hili jipya ni sehemu ya mswada uliotayarishwa na Ujerumani,ambayo hivi sasa imeshika wadhifa wa rais wa Umoja wa Ulaya unaozunguka kila miezi sita.Mawaziri wa nje wa umoja huo wanaokutana leo hii mjini Brussels, wanataka kushughulikia maafikiano ya kuwa na sera moja ya mazingira,ili mpango huo upate kujadiliwa katika mkutano wa kilele juma lijalo.