BERLIN: Msimamo wa Marekani kuhusu mazingira wasikitisha
29 Mei 2007Matangazo
Msemaji wa Baraza la wawakilishi katika bunge la Marekani,Nancy Pelosi anaepingana na Rais George W.Bush kuhusu masuala ya mazingira amekutana na mawaziri wa serikali ya Ujerumani mjini Berlin. Waziri wa mazingira wa Ujerumani,Sigmar Gabriel amesema,anasikitishwa na msimamo wa Marekani wa kutokuwa tayari kuchukua hatua za dhati dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani.