1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Merkel atetea ajenda ya kuhifadhi mazingira

19 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXp

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel ametetea ajenda ya serikali yake iliyo na matumaini makuu ya kuhifadhi mazingira.Alipohojiwa na gazeti la Kijerumani,“Bild am Sonntag“ Kansela Merkel alisema,kila hatua ya kugombea mazingira, isitafsiriwe moja kwa moja kuwa ni mzigo kwa uchumi.Akasisitiza kuwa jumuiya ya kiuchumi hatimae itapata hasara kubwa kama mazingira hayatoshughulikiwa.