1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Bangladesh kuiomba Interpol iwakamate washirika wa Hasina

Angela Mdungu
10 Novemba 2024

Bangladesh imesema itaiomba Polisi ya Kimataifa ya Interpol, iisaidie kuwakamata waliokuwa viongozi katika utawala wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Sheikh Hasina.

https://p.dw.com/p/4mqrL
Sheikh Hasina
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh HasinaPicha: Munir uz Zaman/AFP/Getty Images

Jumapili, mshauri wa masuala ya sheria wa serikali ya mpito Asif Nazul amesema wote waliohusika na mauaji wakati wa maandamano ya Julai na Agosti watarejeshwa  Bangladesh ili wakabiliane na mkono wa sheria.

Soma zaidi: Je, India itamrudisha Sheikh Hasina Bangladesh?

Washirika kadhaa wa Hasina wameshakamatwa tangu utawala wake ulipoanguka, wakituhumiwa kuhusika na operesheni ya polisi iliyowauwa zaidi ya watu 700 wakati wa maandamano yaliyomuondoa madarakani Sheikh Hasina.

Bangladesh tayari imeshatowa waranti wa kukamatwa kwa Waziri Mkuu huyo wa zamani aliyeonekana kwa mara ya mwisho akiwasili India kwa helikopta wakati ambapo waandamanaji waliivamia kasri lake.