1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mkuu wa majeshi wa Bangladesh aapa kuiunga mkono serikali

24 Septemba 2024

Mkuu wa majeshi wa Bangladesh ameapa kuiunga mkono serikali ya mpito kuisaidia kukamilisha mageuzi ya kimsingi, ukiwemo uchaguzi mkuu ndani ya miezi 18, baada ya kuondolewa kwa waziri mkuu wa zamani, Sheikh Hasina.

https://p.dw.com/p/4kzyk
Bangladesh | Jenerali Waker-Uz-Zaman
Mkuu wa Majeshi wa Bangladesh, Waker-uz-Zaman.Picha: DW

Kwenye mahojiano ya kwanza kuchapishwa, Jenerali Waker-uz-Zaman ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba serikali ya mpito inayoongozwa na mshindi wa Tuzo ya Nobel, Muhammad Yunus, inaungwa mkono kikamilifu na jeshi lake na kwamba jeshi halina mpango wowote wa kujiingiza kwenye siasa.

Soma zaidi: Sheikh Hasina akabiliwa na shtaka la mauaji

Jenerali huyo na vikosi vyake walijitenga kando na serikali mapema mwezi wa Agosti wakati wa maandamano ya umma yaliyoongozwa na wanafunzi dhidi ya Hasina, na hivyo kusaidia kuhitimisha utawala wa miaka 15 mwa mwanasiasa huyo mkongwe, aliyekimbilia uhamishoni nchini India.