You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Uchaguzi wa Marekani 2024
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
App
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Misri kurejea kuchimba gesi asilia
Misri imetangaza kuanzisha tena uchimbaji wa gesi asilia ambayo inategemewa kwa kiasi kikubwa ili kuzalisha umeme.
Coca-Cola kuwekeza dola bilioni 1 Nigeria
Kampuni ya Coca-Cola inapanga kuwekeza dola bilioni 1 katika kipindi cha miaka mitano ijayo nchini Nigeria.
Rwanda yaanza chanjo ya Mpox
Rwanda imeanza kutoa chanjo ya ugonjwa wa Mpox kwa watu 300 kwenye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
20.09.2024 - Matangazo ya Asubuhi
Ujumbe wa serikali ya Ukraine uko ziarani Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mji wa Bukavu ambapo umefika kubadilishana fikra na Dk Denis Mukwege+++Mwanasiasa aliyezaliwa Kameruni, Bi. Adeline Abimnwi Awemo, kutoka chama cha Christian Democrat Union, CDU, ndiye mgombea pekee mwenye asili ya Kiafrika kwenye uchaguzi wa jimbo la Brandenburg
19.09.2024 - Matangazo ya Jioni
Israel imeshambulia ngome za wanamgambo wa Hezbollah Kusini mwa Lebanon+++Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) leo kimetoa ripoti inayothmini hali ya demokrasia nchini Tanzania+++Masomo katika vyuo vikuu vya umma nchini Kenya yamekatizwa kutokana na mgomo wa kitaifa wa wahadhiri
19.09.2024 - Matangazo ya Mchana
Awamu mpya ya pili ya mashambulizi ya kielektroniki imeitikisa tena Lebanon na imesababisha vifo vya watu 20+++Wanaharakati, wachambuzi na wadau wa siasa nchini Tanzania, wametoa maoni yao kuhusu kamatakamata ya viongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani Chadema
19.09.2024 - Matangazo ya Asubuhi
Hali ya usalama nchini Mali bado ni tete baada ya waasi kushambulia chuo kimoja cha mafunzo ya kijeshi mjini Bamako +++Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kampuni ya ugavi wa maji ya kunywa mjini Bukavu, REGIDEZO inasema kwamba inashindwa kusambaza kwa wingi maji ya kunywa kutokana na kukauka kwa kiasi kikubwa kwa vyanzo vya maji.
19.09.2024 Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Sikiliza Taarifa ya Habari za Ulimwengu Septemba 19, 2024 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW, Bonn.
18.09.2024 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Blinken ataka usitishaji vita Gaza ili kukomesha machafuko/ Shirika hilo limesema makundi hayo yanaua wanavijiji, watu waliokimbia makazi yao pamoja na waumini wa Kikristo
HRW: Makundi yenye itikadi kali yanawaua raia Burkina Faso
Shirika hilo limesema makundi hayo yanaua wanavijiji, watu waliokimbia makazi yao pamoja na waumini wa Kikristo.
18.09.2024 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Hezbollah yaapa kulipa kisasi mashambulizi dhidi ya Lebanon/ Kundi la itikadi kali ladai kuhusika na mashambulizi, Mali
18.09.2024 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Mafuriko ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika nchi za Nigeria, Cameroon, Niger, Chad, Mali, Ghana na Liberia yamesababisha majanga ya kibinadamu/ Jumla ya mataifa 134 yanayowakilisha asilimia 98 ya uchumi duniani kote yanafikiria juu ya uwezekano wa kutumia sarafu za kidijitali
18.09.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Kwenye Taarifa ya Habari asubuhi ya leo utasikia juu ya mkasa wa kulipuka vifaa vya mawasiliano huko Lebanon na kusababisha vifo vya watu 9 na maelfu kujeruhiwa. Rais Joe Biden wa Marekani aziomba pande zinazozozana nchini sudan kurejea kwenye mazungumzo ya amani na Venezuela yamkamata raia wa 7 wa kigeni kwa madai ya kula njama za kumuua Rais Nicolas Maduro.
17.09.2024 - Matangazo ya Jioni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amelitaka jeshi la polisi nchini humo kuendelea kusimamia maadili ya askari, akisema halipaswi kuhusika au kuhisishwa katika ukiukaji wa haki za sheria+++Viongozi wa vyama vya kihafidhina nchini Ujerumani vya CDU na CSU wamemteua kiongozi wa chama cha CDU, Friedrich Merz, kugombea wadhfa wa kansela wa Ujerumani
Viongozi Asia ya Kati waitaka Ujerumani kuwatambuwa Taliban
Viongozi kadhaa wa mataifa ya Asia ya Kati wameishauri Ujerumani kurejesha mahusiano na utawala wa Taliban.
17.09.2024 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Watu 18 wafariki dunia kutokana na mafuriko barani Ulaya/ Kituo cha mafunzo ya kijeshi Mali chashambuliwa
Demokrasia yashuka ulimwenguni - IDEA International
Idadi ya wapigakura inazidi kushuka na matokeo ya chaguzi yanazidi kutiliwa mashaka katika nchi mbalimbali ulimwenguni.
17.09.2024 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais wa halmashauri kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen ameahidi kumtaja mkuu wa ulinzi kama sehemu muhimu ya timu yake kuu/ Ripoti mpya shirika la kuwasaidia watu wasio na mahala pa kuishi nchini Ujerumani la BAGW imebainisha kuwa, karibu humusi ya watu wasio na makazi ni wenye umri chini ya miaka 25
17.09.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Ungana nasi hapa kusikiliza taarifa ya habari asubuhi ya leo: Uingereza yatumia fedha za mpango wa uhamiaji kulipia teknolojia mpya ya kupambana na magenge ya biashara haramu ya binaadamu. Rais wa Urusi Vladimir Putin ameongeza ukubwa wa jeshi la nchi hiyo Na Idara ya Usalama nchini Marekani kukabiliwa na uchunguzi mpya baada ya jaribio la pili la kuuawa Donald Trump
16.09.2024 Matangazo ya Jioni
16.09.2024 - Matangazo ya Mchana
Baraza la Maaskofu nchini Tanzania, TEC, limekemea matukio ya utekaji na mauaji ambayo yamekuwa yakíendelea kushuhudiwa+++Mtu mmoja amekufa na wengine saba hawajulikani walipo katika Jamhuri ya Czech baada ya kuzuka kwa mafuriko yaliyochochewa na kimbunga Boris
16.09.2024 - Matangazo ya Asubuhi
Katika matangazo yetu ya asubuhi hii utasikia makala zetu za Mbiu ya Mnyonge, Makala yetu Leo, Mtu na Mazingira, Vijana Tugutuke na Jukwaa la manufaa.
16.09.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Ungana nasi hapa kusikiliza Taarifa ya habari ya asubuhi ya leo ambapo habari kubwa miongoni mwa nyingine ni Mgombea wa urais nchini Marekani Donald Trump alengwa na kile ambacho shirika FBI limesema ni jaribio la mauaji: Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine alalama kwamba wanajeshi wake wamepungukiwa silaha: Na Rais William Ruto wa Kenya ajigamba kufanya makubwa katika utawala wake wa miaka miwili.
Ruto atetea rikodi ya uongozi wake wa miaka miwili
Rais William Ruto wa Kenya ametetea rikodi yake ya miaka miwili madarakani katika mahojiano maalumu na DW.
Matangazo ya Jioni: 15.09.2024
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesisitiza kuwa nchi yake haitapeleka makombora ya masafa marefu aina ya Taurus nchini Ukraine. Netanyahu aapa kulipiza kisasi kwa Wahouthi baada ya shambulio la Kombora kuilenga Israel. Watu kadhaa wamekufa kutokana na mafuriko Ulaya ya kati
Matangazo ya Mchana: 15.09.2024
Jeshi la Israel lasema limefanikiwa kuzuia kombora la masafa marefu lililorushwa kuelekea mji wa Tel Aviv likitokea Yemen Jumapili asubuhi. Urusi na Ukraine zashambuliana kwa droni usiku kucha. Watu 18 wameuwawa katika shambulio la kigaidi nchini Somalia
Watu 37 wahukumiwa kifo kwa jaribio la mapinduzi DRC
Mahakama ya Kijeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliwahukumu kifo watu 37, wakiwemo raia watatu wa Marekani.
13.09.2024 - Matangazo ya Jioni
Chama tawala nchini Tanzania, CCM, kimesema kinataka kuona wimbi la vitendo vya utekaji linalokwenda sambamba na mauaji ya raia linamalizika kwa njia ya utulivu na maelewano na siyo kama hatua iliyotangazwa na chama kikuu cha upinzani+++Mamlaka za Ujerumani zimesema zimemkamata kijana mwenye miaka 27 raia wa Syria anayetuhumiwa kupanga shambulio dhidi ya wanajeshi kwa kutumia mapanga.
Msyria mbaroni kwa kutaka kuwauwa wanajeshi Ujerumani
Kijana mwenye miaka 27 raia wa Syria anayetuhumiwa kupanga shambulio dhidi ya wanajeshi amekamatwa Ujerumani.
Afrika katika magazeti ya Ujerumani
Yaliyozingatiwa kwenye magazeti ya Ujerumani juu ya Afrika wiki hii nji pamoja na msaada wa dola bilioni 1.3 kwa Misri uliotolewa na Marekani bila ya kufungamanishwa na hali ya haki za binadamu. Juu ya mvutano baina ya Somalia na Ethiopia kuhusu maji. Ziara ya Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeir nchini Misri. Mtayarishaji ni Zainab Aziz.
Rais wa Senegal atangaza kulivunja bunge
Kiongozi wa Senegal Bassirou Diomaye Faye ametangaza kulivunja bunge la nchi hiyo lenye wapinzani wengi.
13.09.2024 - Matangazo ya Mchana
Jeshi la polisi nchini Tanzania limeyapiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanywa na chama kikuu cha upinzani nchini humo, Chadema, siku ya Septemba 23+++Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye amelivunja bunge la nchi hiyo lenye idadi kubwa ya wabunge wa upinzani.
Oumilkheir atutembelea baada ya miaka minne alipostaafu
Unamkumbuka Oumilkheir? Najua wafuatiliaji wetu wengi "wanaimiss" sauti yake adhimu enzi hizo akiwa nasi hapa Idhaa ya Kiswahili. Baada ya miaka kadhaa tangu alipostaafu, Bi Oumi, kama hapa tulivyopenda kumuita ametutembelea, na kupata fursa ya kuzungumza na mwenzetu John Juma.
12.09.2024 - Matangazo ya Jioni
Marekani imesema hivi leo kuwa itaendelea kuishinikiza Israel kuchukua hatua zaidi ili kuepusha maafa kwenye maeneo ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza+++Kinara wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amekabidhi uongozi wa chama cha ODM kwa gavana wa Kisumu Profesa Peter Anyang Nyong'o.
12.09.2024 - Matangazo ya Mchana
Hali inarejea kuwa ya kawaida katika viwanja vya ndege nchini Kenya baada ya wafanyakazi wa sekta hiyo kuusitisha mgomo uliodumu kutwa nzima hapo jana+++Marekani imesema inaunga mkono kuanzishwa kwa viti viwili vya kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya nchi za Afrika.
11.09.2024 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema upinzani unalitumia swala la uhamiaji kama mtaji wa kisiasa nchini humo/ Wafanyakazi wa uwanja wa ndege Kenya wakubali kusitisha mgomo
11.09.2024 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Mamia ya wafanyakazi katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi JKIA wamegoma dhidi ya mkataba kati ya serikali na mwekezaji wa kigeni/ Harris amkaanga Trump kwenye mdahalo wa televisheni
10.09.2024 - Matangazo ya Jioni
Waziri wa Ulinzi wa Israel amesema makubaliano ya muda ya kusitisha mapigano Gaza yanawezekana lakini akasisitiza kuwa suala la kumaliza vita ni jambo jingine+++Wanaharakati na watendaji katika masuala ya uchaguzi barani Afrika wameelezea utumiaji wa fedha nyingi katika kampeni za uchaguzi ni moaja ya kizingiti katika juhudi za kufanikisha demokrasia.
Mahakama kuu ya Ulaya yaamuru Google na Apple kulipa kodi
Hukumu hii inahitimisha mizozo ya muda mrefu ya kisheria kati ya pande hizo.
10.09.2024 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Wawakilishi wa kundi la mataifa yanayoinukia kiuchumi duniani BRICS wanatarajiwa kujadili juu ya vita vinavyoendelea nchini Ukraine/ Mkutano wa kilele wa kimataifa unaondelea Korea Kusini umetangaza "muongozo wa hatua" zitakazosimamia matumizi na uwajibikaji wa akili mnemba katika jeshi
EU, Marekani: Tutajibu ikiwa Iran inapeleka makombora Urusi
Umoja wa Ulaya umesema umepokea taarifa za kuaminika zinazoonesha kwamba Iran imeipatia Urusi makombora ya masafa.
09.09.2024 Matangazo ya Jioni
Masauni atakiwa kujiuzulu kufuatia kifo cha kada wa CHADEMA+++Ulimwengu uko kwenye njia panda asema Volker Turk+++Papa Francis awasihi viongozi,Timor Mashariki wawalinde watoto dhidi ya unyanyasaji wa kingono+++China yatamba katika michezo ya Olimpiki kwa walemavu Paris
Lishe bora katika kuandaa unyonyeshaji bora
Lishe bora ni kitu cha muhimu wakati mama anapokuwa mjamzito ili kujiandaa kwa ajili ya kumnyonyesha mwanae. Kama wengi tujuavyo, kila mama anahamasishwa kumnyonyesha mtoto wake miezisita ya mwanzo ili kupata lishe bora kabisa anayoihitaji katika ukuaji wake. Kuna mengi ambayo yatakunufaisha ukisikiliza makala ya Afya yako.
09.09.2024 Matangazo ya Mchana
Mwanasiasa wa upinzani 'alietekwa' Tanzania akutwa amekufa+++DNA kufanywa kutambua miili ya waliofariki Endarasha, Kenya+++ Volker Turk azitaka nchi kuchukua hatua dhidi ya Israel+++Ni wakati wa kuishirikisha Urusi kwenye mazungumzo ya kumaliza vita Ukraine - Olaf Scholz
09.09.2024 - Matangazo ya Asubuhi
Katika matangazo yetu ya asubuhi hivi leo utasikia makala zetu za Mbiu ya Mnyonge, Makala yetu Leo, Mtu na Mazingira, Vijana Tugutuke na Jukwaa la manufaa+++Sikiliza ya Dunia Yetu Leo Asubuhi kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW Bonn.
Watu 21 wauawa kwenye shambulizi la sokoni Sudan
Mashambulizi ya makombora yamewaua watu wasiopungua 21 kwenye soko moja kusini mashariki mwa Sudan jana Jumapili.
Mgombea urais wa upinzani Venezuela akimbilia Uhispania
Aliyekuwa mgombea urais wa upande wa upinzani nchini Venezuela Edmundo Gonzalez ameikimbia nchi hiyo.
Matangazo ya jioni: 07.09.2024
Maelfu waandamana Ufaransa kupinga kuteuliwa Barnier kuwa waziri mkuu. Polisi Kenya yaongeza kasi uchunguzi mkasa wa moto shuleni. Wakuu wa ujasusi wa Uingereza na Marekani wasifu shambulizi la Ukraine ndani ya Urusi. Kimbunga Yagi chasababisha vifo vya watu 4 Vietnam.
06.09.2024 - Matangazo ya Jioni
Washirika wa Ukraine wa nchi za Magharibi wanaokutana katika kambi ya kijeshi ya Marekani hapa Ujerumani,wameahidi kuisadia nchi hiyo katika mapambano yake dhidi ya Urusi+++Papa Francis leo Ijumaa amewasili nchini Papua New Guinea baada ya kuhitimisha ziara yake nchini Indonesia.
Afrika katika magazeti ya Ujerumani
Yaliyoandikwa kwenye magazeti ya Ujerumani juu ya Afrika wiki hii ni pamoja na swali lililoulizwa na gazeti la die tageszeitung, jee nani ni rafiki mkubwa kabisa wa China? Juu ya kifo cha mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei. Nchi tano ndizo hasa zinahusika kupeleka silaha zinazokoleza vita nchini Sudan.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 9 wa 130
Ukurasa unaofuatia