Amnesty: Mali ichunguze shambulizi la droni dhidi ya raia
6 Novemba 2024Katika taarifa, Amnesty imesema mashahidi waliripoti kuwa takriban raia wanane, wakiwemo watoto sita, waliuawa katika mashambulizi ya anga kwenye soko lenye shughuli nyingi katika kijiji cha Inadiatafane, katika eneo la Timbuktu, mnamo Oktoba 21.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa watu wengine 15 walijeruhiwa, huku wengine wakiwa katika hali mahututi.
Shambulizi la droni lapaswa kuchunguzwa kama uhalifu wa kivita
Shirika hilo la kutetea haki pia limesema kuwa shambulizi hilo linapaswa kuchunguzwa kama uhalifu wa kivita kwasababu lilisababisha vifo na majeraha miongoni mwa raia huku miundo mbinu ya kiraia pia ikilengwa.
Utawala wa kijeshi Mali wajadili mikakati ya kudhibiti hali ya usalama
Hata hivyo serikali ya Mali haikujibu ombi la tamko kutoka kwa shirika la habari la Ufaransa AFP.
Serikali ya Mali inajitetea dhidi ya shutuma za mara kwa mara za makosa yanayodhuru raia.