Mali yajadili mikakati ya kudhibiti hali ya usalama
24 Septemba 2024Mtawala wa kijeshi nchini Mali kanali Assimi Goita amekutana na maafisa wakuu wa kijeshi nchini humo ili kubadilisha mikakati, baada ya mashambulizi yaliofanywa na makundi ya watu wenye silahakatika mji mkuu Bamako.
Mkutano huo umetoa fursa ya kuangazia upya mipango ya usalama na kuweka mipango ya ziada kuzuia mashambulizi kama hayo siku za usoni.
Kulingana na vyanzo vya usalama, kundi lenye mafungamano na mtandao wa Al-Qaeda lilidai kuhusika na mashambulizi yaliyofanyika Jumanne wiki iliyopita katika mji mkuu Bamako na yaliyolenga sehemu ya uwanja mkuu wa ndege na kambi ya mafunzo ya kijeshi na kuwaua zaidi ya watu 75 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 250.
Soma: Al-Qaeda yadai kumua kamnada Mali
Katika hotuba yake ya kwanza tangu kutokea kwa mashambulizi hayo, kiongozi wa kijeshi Assimi Goita siku ya Jumamosi alitoa risala za rambirambi kwa wahanga wa mashambulizi hayo na kuhimiza umuhimu wa vyombo vya usalama kuwa macho kila wakati.
Wataalamu wamesema mashambulizi hayo yameutikisa utawala huo wa kijeshi ambao umekuwa madarakani tangu mapinduzi ya mwaka 2020 na 2021.