Afrika yakutana kujadili mustakabali wa chakula.
7 Juni 2022Hayo yanakuja kufuatia ongezeko la kupanda kwa bei ya bidhaa katika maeneo mengi duniani kunakosababishwa na vita vinavyoendelea katika nchi za Urusi na Ukraine.
Mkutano wa wakuu hao wa jumuiya za kikanda uliofanyika Arusha Tanzania, yalipo makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ni mkutano wa pili unaowajumuisha viongozi wa wakuuu wa jumuiya sita za kikanda barani Afrika.
Jumuia hiyo ni pamoja na jumuiya ya Afrika Mashariki, jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC, soko la pamoja la Mashariki na kusini mwa Afrika, COMESA, pamoja na jumuiya ya kiuchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika, ECOWAS
Soma pia:Umoja wa Afrika waanza mikutano miwili ya kilele Malabo.
Wakuu hao wamekutana kujadili ajenda ya utekelezaji wa biashara huru barani Afrika,na kuandaa mikakati huru inayotekelezeka. Balozi liberate Mulamula ni waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika wa Tanzania, ameufungua mkutano huo rasmi ambao umehudhuriwa na zaidi ya nchi 40 za Afrika.
Majanga ya kidunia yanawakusanya pamoja viongozi hao
Viongozi wa nchi 44 wa Afrika, walikutana mjini Kigali, Rwanda, mwaka 2018 kwaajili ya kupitisha mkataba wa biashara huru barani Afrika.
Majanga ya kidunia kama vile janga la Corona na vita vya Ukraine na Urusi unawaibua viongozi wa jumuiya za kikanda kutazama fursa za kiuchumi zinazetekelezeka barani Afrika, huku kilimo cha mazao ya chakula ikiwa ni ajenda iliyopewa kipaumbele.
Soma pia:Mkuu wa Umoja wa Afrika amwambia Putin, Waafrika ndio 'waathirika' wa mzozo wa Ukraine
Jumuiya ya Afrika Mashariki imekuwa mwenyeji wa mkutano huu kwa mara ya kwanza ambayo inakubali kuwa hiyo ni changamoto kubwa ambayo inalikumba bara la Afrika lakini kwa mtazamo mwingine ni fursa.
Dr. Peter Mathuki ni katibu mkuu wa juiya ya Afrika Mashariki amesema mkutano huuunafanyika ukilenga kusaka suluhu ya changamoto hizo kwa kushirikisha vema sekta binafsi.
"Tuwezeshe wanawake na vijana tutaweza piga kumbo umasikini huu" Aliwaambia waandishi wa habari katibu mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki Dr. Mathuki.
Masuala ya kuondolewa kwa vikwazo vya kibiashara pamoja usafirishaji wa bidhaa miongozi mwa nchi za Afrika, ni ajenda pia zilizojadiliwa kwenye mkutano huo ambao unakuja wakati mataifa mengi ya pembe ya Afrika yakitajwa kukabiliwa na njaa pamoja na ukame.
masuala ya ushirikishwa wa vijana na wanawake katika utekeleza mkataba huo ukizingatiwa kwa kiwango cha juu. Mkutano huo wa siku nne, utatoka na maazimio ambayo yatawasilishwa kwa wakuu wan chi za Afrika kwaajili ya kupitishwa na kufanyiwa utekelezaji.