Vifo kutokana na COVID kupungua Afrika kwa asilimia 94, WHO
2 Juni 2022Janga hilo lilikuwa hatari sana katika bara la Afrika mwaka wa 2021, ambapo lilishikilia nafasi ya saba baada ya Malaria miongoni mwa magonjwa yanayoongoza katika kusababisha vifo barani humo.
"Tathmini yetu ya hivi karibuni inabashiri kuwa vifo kutokana na Covid barani Afrika vitapungua hadi asilimia 60 kila siku mwaka 2022… Mwaka uliopita, tulipoteza kwa wastani watu 970 kila siku barani humo,” amesema Matshidiso Moeti, Mkurugenzi Mtendaji wa WHO barani Afrika kwenye mkutano wake na waandishi wa habari kwa njia ya video.
Kenya yaondoa masharti ya mwisho ya Covid-19
Kushuka kwa takwimu hizo kumesababishwa na ongezeko la watu kupokea chanjo, juhudi zilizoimarishwa kupambana na janga lenyewe pamoja na kinga ya kawaida mwilini dhidi ya maambukizi ya zamani, WHO imesema.
Vifo Afrika kufuatia COVID havikuwa vingi ikilinganishwa na baadhi ya mabara.
Nchi tajiri za magharibi pamoja na nchi za kusini mwa Afrika zilikuwa na vifo maradufu ikilinganishwa na vifo katika nchi maskini na maeneo mengine ya Afrika. Kwa sehemu fulani, hali hiyo ilitokana na magonjwa yanayoongeza hatari ya kifo. Hayo ni kulingana na tathmini ya WHO.
Kwa wajane Afrika, COVID-19 iliiba waume, nyumba, mustakablali
Kulingana na tathmini ya WHO, takriban vifo 23,000 vinatarajiwa kutokea ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, ikiwa hali ya maambukizi itaendelea kama ilivyo sasa.
Tathmini hiyo imeeleza kuwa ni kisa kimoja tu cha maambukizi miongoni mwa visa 71 vya COVID-19 hurekodiwa barani Afrika na kwamba moja kati ya vifo vitatu hukosa kurekodiwa.
Nchi nyingi Afrika hazikuweka rekodi sahihi
Ingawa nchi nyingi za Afrika zilitatizika mwanzoni mwa janga hilo, kupata chanjo, huku nchi tajiri zikizihodhi dozi zilizokuwepo, (WHO yakemea kukosekana kwa usawa katika usambazaji wa chanjo)
kwa sasa nchi nyingi barani humo zina chanjo ila changamoto ni kuhakikisha watu wamechanjwa, ikizingatiwa baadhi wanachelea kukubali chanjo na vilevile taratibu za kuwafikia watu.
Mwishoni mwa mwezi Mei, Afrika ilikuwa imeripoti zaidi ya maambukizi ya COVID yaliyothibitishwa milioni 1.8, na zaidi ya vifo 250,000.
"Kazi haijamalizika. Kila tunapolegeza kamba, maambukizi ya COVID-19, huongezeka tena. Kitisho cha aina mpya ya maambukizi kingalipo na tunapaswa kuwa tayari kupambana na hatari hii ambayo daima iko nasi,” Moeti aliwaambia waandishi habari.
(RTRE)