Uamuzi wa utata wapelekea kuondolewa kwa afisa wa VAR
30 Novemba 2023Afisa aliyesimamia teknolojia ya video VAR kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa, Tomasz Kwiatkowski ameondolewa kwenye nafasi yake ikiwa ni siku moja baada ya kufanya uamuzi wa kuwapa Paris Saint-Germain penalti katika dakika za mwisho, kufuatia mpira kuguswa na mkono walipocheza dhidi ya Newcastle.
Rais huyo wa Poland Tomasz Kwiatkowski ameondolewa kusimamia mechi ya Real Sociedad dhid ya Salzburg na nafasi yake imechukuliwa na muamuzi mwingine kutoka Ujerumani.
Soma pia: Shirika la mazingiria la Ujerumani lakosoa kombe la dunia 2030 nchi sita
Mshambuliaji Kylian Mbappe alifunga bao dakika ya mwisho wa mchezo na kuisadia PSG kutoka sare ya 1-1 baada ya mpira kumpiga beki wa Newcastle, Tino Livramento kifuani kisha kutua mkononi mwake, tukio lililopelekea penalti kutolewa na mwamuzi huyo baada ya kutizama marudio kwenye VAR.
Awali Marciniak aliruhusu mchezo uendelee, lakini baada ya kushauriwa na msaidizi wake wa video kukagua tukio hilo kwenye VAR.
Uamuzi wa penalti katika mchezo wa PSG umeathiri moja kwa moja msimamo wa Kundi F kwa kuwaweka PSG katika nafasi ya pili, alama mbili mbele ya Newcastle. Kundi hilo linaongozwa na Borussia Dortmund.
Meneja wa Newcastle Eddie Howe ameeleza kutoridhishwa na uamuzi huo wa penalti.
Ili kufuzu hatua ya 16 bora, Newcastle kwa sasa inalazimika kupata ushindi kwenye mchezo wake wa nyumbani dhidi ya AC Milan mnamo Desemba 13 ikitegemea PSG isipate ushindi katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Borrusia Dortmund.