1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZURICH:Cannavaro ndie mchezaji bora wa soka mwaka huu

19 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCiO

Katika michezo Kaptein aliyeiongoza timu ya Italy katika mashindano ya kandanda ya kombe la Dunia hapa ujerumani mwaka huu Fabio Cannavaro ametunzwa tunzo ya FIFA ya mchezaji bora wa mwaka.

Cannavaro ametunukiwa tunzo hiyo baada ya kupigiwa kura ambapo Zinedine Zidane alikuwa wa pili akifuatiwa na Ronaldinho.

Akipokea tunzo hiyo Cannavaro ambaye anachezea Real Madrid alisema kimekuwa ni kinyang’anyiro kigumu hasa ukizingatia kuweko kwa Ronaldinho na Zidane.

Kwa upande wa kina dada aliyetunukiwa tuzo hiyo ni mbrazil Marta aliyefuatiwa na mjerumani Renate Lingor na Mmarekani Kristine Lilly akawa wa tatu.