1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Nigeria

Hawa Bihoga
27 Februari 2023

Zoezi la kuhesabu kura katika uchaguzi mkuu nchini Negeria linaendelea ingawa mashambulizi kadhaa katika baadhi ya nchi hiyo ya Afrika magharibi yalichelewesha mchakato huo wa kidemokrasia.

https://p.dw.com/p/4O15B
Nigeria | Auszählung Wahlen
Picha: Sunday Alamba/AP Photo/picture alliance

Matokeo kutoka katika idadi kubwa ya vituo vya kupiga kura kote nchini humo yapo katika mchakato wa kujumuishwa, baada ya ucheleweshwaji mkubwa na kushuhudiwa mashambulizi katika baadhi ya vituo vya kupiga kura siku ya Jumamosi, hatua iliolazimu kuhairishwa kwa mchakato hadi Jumapili.

Nigeria yapiga kura kuchagua rais na bunge

Polisi nchini humo imethibitisha kutokea kwa mashambulizi hasa katika mji mkuu wa kibiashara Lagos.

Takriban wapigakura milioni 87.2 walikuwa na vigezo vya kupiga kura ya kumchagua mrithi wa rais Muhammadu Buhari aliehudumu kwa mihula miwili, huku changamoto ya maisha bora,vurugu za makundi ya uasi pamoja na mzozo wa noti vikiwa miongoni mwa vibarua vigumu kwa rais ajae wa Nigeria.