1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zimesalia siku 100 kuanza kwa olimpiki Beijing

Kalyango Siraj30 Aprili 2008

Mwenge umerejea China baada ya safari ya nchi 20

https://p.dw.com/p/DrC3
Watazamaji wakipeperusha bendera za China katika moja wa barabara za mji wa Japan wa Nagano, Jumamosi April 26, 2008 wakati wa mbio za mwenge wa Olimpiki itakayofanyika Beijing kuanzia Agosti 8. Mwenge huo sasa umerejea China na kwa sasa unahifadhiwa katika kisiwa cha Hong Kong.Picha: AP

Zikiwa zimebakia siku 100 ili michezo ya Olimpiki ya mwaka huu kuanza nchini China, mwenge wa michezo hiyo ambao umekimbizwa katika nchi 20 sasa umerejea tena katika ardhi ya China, mara hii katika kisiwa cha Hong Kong.

Siku ya leo imeanza kwa dua ya kumuomba Maulana abariki China pamoja na michezo ya Olimpiki ifanyike kwa amani.

Dua hiyo imeombwa na Askofu mpya wa dini ya kikatoliki wa Beijing Joseph Li Shan.Askofu huyo alikuwa anaongoza ibaada maalum ya leo ikiwa zimesalia siku 100 ili kwa mji huo kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki ya mwaka huu.

Michezo imepangwa kuanza Agosti 8 na kumalizika Agosti 24.

Mji huo utakuwa mwenyeji wa michezo 37 ,huku michezo 28 itakuwa ya kuwania medali na mingine iliosalia itakuwa ya mazoezi.

Mbali na sala maalum shughuli zingine za kuadhimisha siku hii ni mbio za marathon za kielelezo ambapo watu maelfu kadhaa wameshiriki.

Sherehe zimefanyika karibu na mahali patakapofanyika sherehe kuu za ufunguzi wa michezo hiyo kaskazini mwa mji wa Beijing.

Baadae leo jumatano kutafanyika sherehe katika uwanja wa Tiannamen ambayo itatangazwa moja kwa moja kupitia televisheni kwa watazamaji wengi dunaini.

Katika sherehe hiyo inatazamiwa kuzinduliwa rasmi wimbo wa mada ya michezo hiyo.

Siku hii pia imebarikiwa kutokana na mwenge wa michezo hiyo kurejea tena katika ardhi ya China baada ya safari ndefu ya nchi 20 safari iliogubikwa na maandamano dhidi ya China inavyokiuka haki za binadamu.

Lakini baado kuna kiwingu cha maandamano dhidi ya suala la Tibet.

Mwenge huo umewekwa mahali pa siri hadi Ijumaa ambapo utaanza mbio za ndani mwa China.Wadadisi wanasema huenda ukakabilina na maandamano sio tu katika maeneo ya Tibet lakini pia ya Xinjiang kwenye waislamu wengi .Nako huko inasekema utawala wa China unachukiwa kwa kiasi kutokana na hatua za udhibiti wa dini hiyo.

Mbali na hayo kuna masuala mengine ambayo baado hayajasuluhiswa kwa ajili ya michezo hiyo ya Beijing.

Miongoni mwa masuala hayo ni lile la vumbi katika jiji hilo.Suala ambalo limewafanya baadhi ya wanariadha kama vile haile Gebraselassie kusema kuwa hawatashiriki katika michezo hiyo kutokana na uchafuzi wa mazingira ambao unaweza kuhatarisha maisha yake.

Suala lingine pia ni la ukandamizaji wa vyombo vya habari.Katika taarifa iliotolewa leo jumatano, chama cha wandishi wa habari wa mashirika ya kigeni nchini humo kimeonya kuwa ikiwa mtindo dhidi ya waandihi habari hautakoma huenda jambo hilo likatia doa na kutoa hisia mbaya katika ulimwengu wa wandishi wa habari kutoka nchi za nje sana sana watakaokuwa wanataka kuripoti michezo hiyo.