1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zimbabwe

Oumilkher Hamidou4 Januari 2009

Mwanaharakati wa haki za binaadam nchini Zimbabwe alishwa sumu jela

https://p.dw.com/p/GRp2

Johannesburg:


Mwanaharakati mashuhuri wa haki za binaadam,Jestina Mukoko,anaeshikiliwa jela kwa tuhuma za kuandaa njama dhidi ya rais Robert Mugabe,anasemekana amelishwa sumu.Hayo ni kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini humo.Gazeti la Sunday Independant,bibi Mukoko,anaeshikiliwa peke yake katika jela ya ulinzi wa hali ya juu ya Chikurubi,amelishwa sumu na watumishi wa jela hiyo.Wakili wake,Beatrice Mtetwa ametaka uchunguzi ufanywe kabla ya kutuma mashtaka mahakamani.Jestina Mukoko,mkurugenzi wa shirika lisilo milikiwa na serikali la Zimbabwe Peace Project-ZPP alitekwa nyara  nyumbani kwake na watu waliokua na silaha,december tatu mwaka jana na kushikiliwa mahala pasipojulikana kwa wiki kadhaa.Alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza December 24 iliyopita.Ijumaa iliyopita,korti imekataa shauri la kupelekwa kwake hospitali.Mwanaharakati huyo alikua akichunguza machafuko ya kisiasa yaliyoripuka wakati wa uchaguzi uliopita na kugharimu maisha ya zaidi ya watu 100.